Bwawa lililovunjika hapo Septemba 10, lilisababisha mafuriko makubwa ambapo watu kadhaa walipoteza maisha na zaidi ya milioni moja kukoseshwa makazi, na kusababisha kuhamisha watu kote katika jimbo la Borno ..
Msemaji wa idara ya magereza ya Nigeria Umar Abubakar alisema Jumapili usiku kuwa maafisa walijaribu kuwahamisha watu kutoka katika gereza kuu ambalo liko kwenye mji wa Maiduguri, baada ya kugundua kuwa wafungwa walikuwa wametoroka.
Alisema kuwa mafuriko hayo yaliangusha kuta za jela hiyo kikiwemo kituo cha usalama, pamoja na makazi ya maafisa wa jela. Maafisa wa usalama walifanikiwa kuwapata wafungwa 7 miongoni mwa waliotoroka, wakati operesheni ya kuwasaka waliobaki ikiendelea.
Kuvunjika kwa bwawa hilo kumesababisha mafuriko mabaya sana yanayoweza kulinganishwa na yale ya miaka 30 iliyopita. Afrika Magharibi imeshudia mafuriko mabaya zaidi mwaka huu ndani ya miongo kadhaa, ikiwa yameathiri zaidi ya watu milioni 2.3, ikiwa ni mara tatu zaidi, ikilinganishwa na mwaka uliopita, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Forum