Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:06

Yellen aanza ziara ya siku kumi barani Afrika kujadili mikakati ya kukuza uchumi


Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen

Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen ameanza ziara ya siku kumi barani Afrika ili kujadili mikakati ya ukuaji wa uchumi na kuthibitisha tena nia ya dhati ya Marekani kuimarisha uhusiano na bara hilo.

Alianza ziara yake kwakutembelea biashara inayofadhiliwa na Marekani ya kutotoa vifaranga kwa ajili ya vijana na wanawake mjini Dakar, nchini Senegal.

Akiwa ni mwanamke wa kwanza waziri wa fedha Marekani, Yellen alipata ukaribisho mzuri kutoka kwa wafanyabaishara wanawake katika mkutano wa Ijumaa.

Katika hotuba yake kufuatia ziara hiyo, Yellen alisisitiza azma ya Marekani kupanua biashara na uwekezaji barani Afrika. “Marekani iko ndani Afrika na iko pamoja na Afrika. Kujihusisha kwetu si suala la kimikataba. Siyo tu kujionyesha. Na siyo kwa muda mfupi,” aliongezea Yellen.

Ziara ya Yellen imekuja baada ya mkutano wa mwezi uliopita wa viongozi wa Marekani na Afrika, ambapo Rais Joe Biden aliahidi kiasi cha dola bilioni 55 za misaada katika uchumi, afya na usalama kwenye bara hilo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Wajumbe kadhaa wa utawala wa Biden, kama vile Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken na mwakilishi maalum wa hali ya hewa John Kerry, tayari walisafiri kwenda Afrika. Rais Biden, mke Jill Biden na makamu rais Kamala Harris pia wanapanga kufanya ziara barani humo.

Kujihusisha kwa Marekani barani Afrika kulichukua nafasi ya nyuma wakati wa utawala wa Trump. Wakati huo huo, Beijing inawekeza mabilioni katika miradi ya miundo mbinu ya Afrika na kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara na Afrika, wakati kundi la kijeshi linaloungwa mkono na Russia liko kote katika bara hilo.

Ziara ya Yellen inatuma ujumbe wa wazi kwamba Marekani iko tayari kushindana.

Afrika ni nyumbani kwa akiba kubwa sana ya madini duniani ambayo ni muhimu kwa mipango ya utawala wa Biden kuhamasisha nishati safi.

Sarah Danzman ni profesa wa masuala ya kimataifa katika chuo kikuu cha Bloomington, Indiana anasema, “Marekani inataka kusisitiza kwamba uwekezaji wa Marekani ni bora zaidi na kuaminika katika kushirikiana ukuaji na ustawi kote katika bara hilo, hasa kwasababu ni wazi, ukiendana na thamini za demokrasia na haki za binadamu na pia kuhusishwa na mageuzi ya utawala kupunguza rushwa,” ameongezea.

Hayo ni kinyume kabisa na mfano wa uwekezaji wa wachina, ambao umeweka kipaumbele kwa ujenzi wa haraka na uchimbaji wa rasilimali juu ya mahitaji ya utawala mzuri aliongezea.

wakati akiwa nchini Senegal, Yellen pia atatembelea kituo kilichokuwa cha biashara ya utumwa kwenye kisiwa cha Goree na kukutana na Rais wa Senegal na mkuu wa Umoja wa Afrika, Macky Sall pamoja na mawaziri wa fedha na uchumi.

Anapanga kujadili ushirikiano katika miradi ya miundo mbinu, kujitayarisha kwajanga, kuimarisha demokrasia na mapambano ya rushwa. Pia ataangazia hatua ambazo zimechukuliwa na Marekani kukabiliana na athari za vita vya Russia nchini Ukraine kwa njia ya kutoa misaada ya usalama wa chakula.

Yellen anasema “Vita vya Russia na matumizi ya chakula kama silaha yamezidisha ukosefu wa usalama wa chakula na kusababisha madhila yasiyoelezeka. Wakati matatizo ya kiuchumi ulimwenguni yalisababishwa na hatua za mtu mmoja tu, Rais Putin inauvuta uchumi wa Afrika isivyo stahili.”

Yellen pia alikiri Afrika pia ina changamoto za mzozo wa hali ya hewa, akielezea kwamba nchi 17 kati ya 20 za juu duniani zilizo katika mazingira hatarishi ya hali ya hewa ziko barani Afrika.

Alitangaza mipango ya Marekani kupanua ushirikiano na AFrika kuhusu uhifadhi, kukabiliana na hali ya hewa na fursa kwa nishati safi, na alielezea azma ya Biden kutoa zaidi ya dola bilioni moja kusaidia juhudi zinazoongozwa na Afrika katika kukabiliana na hali ya hewa.

Yellen alikiri kuwa mchango wa Marekani kwenye ujenzi wa kiwanda kikubwa cha upepo huko Afrika Magharibi, kiko nje ya Dakar.

Jumamosi atakwenda kwenye mradi mkubwa sana wa umeme vijijini unaofadhiliwa na Marekani ambayo unaongozwa na kampuni ya uhandisi ya Marekani.

Baada ya Senegal, Yellen ataendelea na ziara yake nchini Zambia na Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG