Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:08

Winnie Mandela atoka hospitali Afrika Kusini


İranın ali ruhanisi Ayətullah Əli Xamenei İranda prezident seçkisində iştirak edir. 
İranın ali ruhanisi Ayətullah Əli Xamenei İranda prezident seçkisində iştirak edir. 

Mwanaharakati mkongwe wa Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela aliyepigania kuondolewa ubaguzi wa rangi Africa Kusini ameruhusiwa kutoka hospitali siku ya Jumanne.

Winnie alikuwa anatibiwa figo iliyokuwa ina matatizo, msemaji wa familia ya Mandela amesema katika tamko lake.

Madikizela-Mandela alilazwa katika hospitali ya Milpark Johannesburg siku 10 zilizopita. Amekuwa akipokelewa hospitalini na kuruhusiwa tangu mwaka 2016 kwa matibabu ya mgongo na goti.

“Nimefurahi kuruhusiwa kwenda nyumbani ambapo nitaweza kupumzika na kurejesha kikamilifu hali yangu kutokana na maradhi ya muda mfupi,” tamko hilo limemkariri Madikizela-Mandela.

Wakati mtalaka wake alipokuwa anatumikia kifungo cha miaka 27 kwa ajili ya kupinga ubaguzi wa rangi , Madikizela-Mandela alifanya kampeni kushinikiza atolewe jela na kupigia kelele haki za Waafrika weusi nchi Afrika Kusini, na alikamatwa na kupigwa marufuku nchini. Utawala wa wazungu wachache ulifikia kikomo mwaka 1994.

XS
SM
MD
LG