Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:59

Bajeti ya WHO ya dola bilioni 6.83 yakubaliwa na kamati kuu


PICHA YA MAKTABA: Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
PICHA YA MAKTABA: Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus

Shirika la Afya duniani (WHO) Jumatatu lilipewa kibali cha  bajeti ya dola bilioni 6.83 kwa kipindi cha miaka miwili ijayo, ikijumuisha kupandisha asilimia 20 ya ada za lazima ya uanachama.

Wakati shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika masuala ya afya likianza mkutano wake wa kila mwaka wa kufanya maamuzi, mataifa wanachama katika kamati kuu yalipitisha bajeti hiyo bila pingamizi.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, alipongeza hatua hiyo kama kwa kuita ya kihistoria na hatua kubwa.

Bajeti hiyo bado inahitaji kuidhinishwa na nchi zote wanachama mwishoni mwa tukio hilo la siku 10 lakini utaratibu wa kuidhinisha kimsingi ni kwa ajili ya utaratibu tu.

Uamuzi huo umefanyika baada ya mkutano wa mwaka jana kukubali kufanya marekebisho makubwa ya ufadhili wa WHO.

Baada ya kusumbuliwa na janga la COVID-19, mataifa yalikubaliana juu ya uhitaji wa kutoa ufadhili wa kuaminika na wenye uthabiti.

WHO inafadhiliwa kwa kiasi kikubwa na nchi wanachama 194.

Sehemu ya ufadhili kutoka ada ya lazima ya uanachama yaani michango iliyokadiriwa ilipigiwa hesabu kulingana na utajiri na idadi ya watu ilipungua mpaka chini ya moja ya tano na iliyobaki ikitoka kwa michango ya hiari.

Hali hii imeifanya WHO kuwa na mwanya mdogo wa kushughulikia majanga kama vile COVID-19, vita vya Ukraine na dharura zingine za kiafya.

Mkutano wa mwaka jana ulikubali kuongeza hatua kwa hatua sehemu ya ada ya wanachama hadi asilimia 50 itakapofikia bajeti ya 2030 – 2031.

XS
SM
MD
LG