Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 01:21

Zima Moto wapambana kuzima moto majengo ya Bunge Cape Town


Moto ukiwaka katika jengo moja la Bunge la Taifa Cape Town, Jan. 2, 2022. (AP Photo/Jerome Delay)
Moto ukiwaka katika jengo moja la Bunge la Taifa Cape Town, Jan. 2, 2022. (AP Photo/Jerome Delay)

Kikosi cha zima moto kimepambana na moto uliozuka katika majengo ya Bunge la taifa nchini Afrika Kusini Jumapili uliosababisha wingu nene la moshi na miale ya moto kutanda hewani mjini Cape Town.

Moto ulianzia katika ghorofa ya tatu ya jengo lenye ofisi na kuenea hadi katika jengo la Bunge la Taifa, ambako Bunge la Afrika Kusini hukutana, Waziri wa Ujenzi na Miundombinu Patricia de Lille alisema.

“Moto hivi sasa unawaka katika ukumbi wa Bunge la Taifa,” Waziri De Lille alisema. “Hii ni siku ya masikitiko makubwa kwa demokrasia, Bunge ni makazi ya demokrasia yetu.”

Msemaji wa huduma za zimamoto na uokoaji mjini Cape Town Jermaine Carelse amesema hakuna majeruhi yaliyoripotiwa. Walinzi kwanza walitoa taarifa kuhusu moto huo majira ya saa kumi na mbili asubuhi , amesema, na wafanyakazi 35 wa zima moto walikuwa katika eneo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amejulishwa kuhusu moto huo, De Lille alisema. Rais na wanasiasa wengi wa ngazi ya juu walikuwa Cape Town kwa ajili ya mazishi ya Askofu Mkuu Desmond Tutu, yaliyofanyika Jumamosi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George mjini humo, ambalo liko mtaa moja kutoka katika eneo la Bunge.

Moto huo mwanzoni ulioonekana kuwaka katika jengo la zamani la Bunge lililoko nyuma ya Bunge la Taifa, De Lille amewaambia waandishi awali ni kwenye milango ya mbele ya majengo ya Bunge. Kabla hajatangaza kuwa moto huo ulikuwa umeenea katika majengo ya Bunge la Taifa, alisema kuwa kuwa zimamoto “ walikuwa wameidhibiti hali hiyo.”

Maafisa walikhofia kwamba sehemu ya majengo, baadhi yake yalikuwa yamejengwa katika miaka ya 1800, yanaweza kuanguka kwa sababu ya joto kali.

“Lami ambayo iko juu ya paa inayayuka, ni dalili ya kuwepo joto kali. Kumekuwa na taarifa kuwa baadhi ya kuta zinaonyesha ufa, huenda inaashiria kuanguka kwake,” Tovuti ya News24 imemkariri Carelse akielezea.

Polisi wamelizingira eneo la majengo na barabara zote. Baadhi ya maeneo yaliyofungwa ni yale yaliyokuwa karibu na sehemu ambako watu waliacha maua na salamu za rambirambi kwa ajili ya Tutu.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters

XS
SM
MD
LG