Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:31

Afrika kusini imeanza maombolezo ya Desmond Tutu hadi siku ya mazishi


Maombolezo ya askofu Desmond Tutu kwenye kanisa la St. George's Cathedral huko Cape Town, South Africa, Dec. 26, 2021.
Maombolezo ya askofu Desmond Tutu kwenye kanisa la St. George's Cathedral huko Cape Town, South Africa, Dec. 26, 2021.

Kila siku saa sita mchana kengele katika kanisa kuu la St. George’s mjini Cape Town zitalia kwa dakika 10. Kitabu cha wageni kimewekwa katika kanisa kuu kwa waombolezaji kutia saini. Ukumbi wa jiji la Cape Town na Table Mountain utawashwa taa za  rangi ya zambarau kila usiku hadi siku ya mazishi

Afrika kusini itakuwa na maombolezo ya wiki moja kuelekea mazishi Jumamosi wakati wa mazishi ya Askofu mkuu Emeritus Desmond Tutu aliyefariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 90.

Kila siku saa sita mchana kengele katika kanisa kuu la St. George’s mjini Cape Town zitalia kwa dakika 10. Kitabu cha wageni kimewekwa katika kanisa kuu kwa waombolezaji kutia saini. Ukumbi wa jiji la Cape Town na Table Mountain, pia utawashwa taa za rangi ya zambarau kila usiku hadi siku ya mazishi.

Baadhi ya watu wakipiga picha kwenye sanamu ya Desmond Tutu Dec. 26, 2021.
Baadhi ya watu wakipiga picha kwenye sanamu ya Desmond Tutu Dec. 26, 2021.

Desmond Tutu mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel alijulikana duniani kote kwa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi na kama mtetezi wa haki za binadamu mwili wake utawekwa katika jimbo hilo kwenye kanisa kuu hapo Ijumaa.

Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa alitangaza kifo cha Tutu jana Jumapili. "Kufariki kwa Askof Mkuu Emeritus Desmond Tutu ni ukurasa mwingine wa msiba uliolikumba taifa letu katika kuaga kizazi cha wa-Afrika kusini mashuhuri ambao wametuachia urithi wa Afrika kusini iliyokombolewa" alisema. Tutu alikuwa zaidi ya kiongozi wa kiroho. Maisha yake yote aliyatumia kutetea haki za kiraia na kuzungumza dhidi ya ukosefu wa sheria, rushwa na uonevu.

XS
SM
MD
LG