Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:44

Watu zaidi ya 8 wauwawa shuleni Texas


Shule ya sekondari ya Santa Fe, Texas, Marekani
Shule ya sekondari ya Santa Fe, Texas, Marekani

Sio chini ya watu wanane wameuwawa katika tukio la shambulizi la bunduki Ijumaa asubuhi huko Shule ya Sekondari ya Santa Fe katika eneo la Santa Fe, Texas, kwa mujibu wa mkuu wa polisi kaunti ya jirani ya Harris Ed Gonzalez .

“Inawezekana ikawa ni kati ya watu 8 mpaka 10 waliouwawa, wengi wao ni wanafunzi,” Gonzalez pia amesema, “mshukiwa huyo anayeshikiliwa mahabusu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi.”

Uongozi wa shule ya kujitegemea ya Santa Fe (ISD) amesema katika tamko kuwa watu wamejeruhiwa lakini hakueleza idadi yao.

Gonzalez amesema afisa wa polisi mmoja ni kati ya wale waliojeruhiwa na “na haijulikani ni kwa kiasi gani ameumizwa.”

Rais Donald Trump ameeleza shambulizi hilo kuwa “ hakuna shaka ni shambulizi la kinyama,” moja ya mashambulizi mengi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu nchini.”

Trump amewaambia walioathirika na shambulizi hili na familia zao “sisi tuko pamoja na nyie katika saa hii ya msiba huu na tutaendelea kuwa na nyinyi milele.” Aliahidi kuondoa silaha “ kutoka mikononi ma wale wanaohatarisha maisha yao na ya watu wengine.

XS
SM
MD
LG