Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:18

Shambulizi la bunduki lauwa Shuleni Texas


Ramani ya eneo la shambulizi huko Texas.
Ramani ya eneo la shambulizi huko Texas.

Watu kadhaa wameuwawa katika shambulizi la kutumia risasi za moto katika shule ya sekondari ya Santa Fe, Texas, imetokea Ijumaa, kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya eneo hilo.

Uongozi wa shule hiyo umesema kuwa kuna majeruhi katika shambulizi hilo, lakini hawajatoa idadi yao.

Wamiliki wa Shule ya kujitegemea ya Santa Fe (ISD) wametoa tamko kuwa "hali fulani imetokea katika shule hiyo ambapo kulikuwa na mshambuliaji aliyetumia bunduki.

Tayari uongozi umeweka vizuizi katika eneo hilo.

Polisi na wahudumu wa masuala ya dharura walipelekwa katika eneo la tukio, pamoja na wawakilishi wa serikali kuu kutoka katika kitengo kinachokabiliana na Ulevi, Tumbaku, Silaha na Mabomu.

Santa Fe iko katika eneo la kusini mashariki ya Texas kati ya mji wa Houston na Galveston.

XS
SM
MD
LG