Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:09

Watu 48 wafariki katika mlipuko wa lori la mafuta kaskazini mwa Nigeria


Wapita njia wakikusanyika kwenye eneo ambako lori la mafuta lilipinduka na kusababisha moto mkubwa mjini Lagos, Februari 18, 2012.
Wapita njia wakikusanyika kwenye eneo ambako lori la mafuta lilipinduka na kusababisha moto mkubwa mjini Lagos, Februari 18, 2012.

Takriban watu 48 walifariki Jumapili katika mlipuko wa lori la kubeba mafuta baada ya kugongana na gari nyingine katika jimbo la Niger lililo eneo la kati, la kaskazini mwa Nigeria, idara ya kusimamia majanga katika jimbo hilo imesema.

Idara hiyo imesema lori hilo la mafuta liligongana na lori lililokuwa linasafirisha watu na mifugo. Magari mengine kadhaa yalijikuta katika ajali hiyo, idari hiyo imesema.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba magari mengine mawili, lori la kubeba na kunyanyua mizigo na gari la kubeba mizigo yalihusika katika ajali hiyo na kuwaka moto.

Msemaji wa idara hiyo ya majanga Hussaini Ibrahim alisema idadi ya waliofariki ni 48 na maafisa walikuwa wakijaribu kuondoa magari hayo kwenye eneo la tukio.

Kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali NNPC wiki iliyopita iliongeza bei ya petroli kwa asilimia 39, ikiwa ni ongezeko kubwa la pili kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini uhaba wa mafuta umeendelea, na kuwalazimu madereva kupanga foleni kwa saa kadhaa katika miji na miji mikubwa ya nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG