Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:30

Watu 23 wauawa katika shambulizi nchini Mali


Maafisa wa usalama nchini Mali.
Maafisa wa usalama nchini Mali.

Watu wenye silaha wamewaua takriban watu 23, na kujeruhi 12 katika shambulio lililofanywa katika kijiji kimoja katikati mwa Mali, maafisa walisema Jumapili.

Sidi Mohamed El Bechir, gavana wa jimbo la Bandiagara ambako shambulio hilo lilifanyika, alisema watu wasiojulikana waliua darzeni za watu Ijumaa na kuchoma moto nyumba kadhaa katika kijiji cha Yarou.

“Washambuliaji walikaa kijijini hapo hadi saa 7 mchana, na kuteketeza sehemu ya kijiji, kuvunja maduka na kuchukua ng’ombe wa wanakijiji,” alisema Amadou Lougue, rais wa shirika la vijana la kieneo siku ya Jumapili.

Hadi tulipokuwa tukitayarisha ripoti hii, hakuana aliyekuwa amendai kuhusika na shambulio hilo

Jamii za eneo la kati na kaskazini mwa Mali zimekuwa katika mzozo wa ghasia za muda mrefu za kutumia silaha tangu mwaka 2012.

Waasi wenye itikadi kali walilazimishwa kuondoka madarakani katika miji ya kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Magharibi mwaka uliofuata, kwa msaada wa operesheni ya kijeshi iliyoongozwa na Ufaransa.

Lakini walijikusanyika tena jangwani na kuanza kushambulia jeshi la Mali na washirika wake.

Shambulio la Jumapili katika eneo la kati la Mopti, lilifanyika siku ambapo jeshi la Mali lilishutumu watu wenye itikadi kali wenye silaha kwa kurusha roketi iliyolenga mji wa magharibi wa Timbuktu, takriban kilomita 275 kaskazini mwa mwa Bandiagara.

Forum

XS
SM
MD
LG