Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 21:50

Wajasirimali wa nchi za Afrika wafurahia nafasi za kuingia China


Mfanyakazi katika kiwanda cha kutengeneza paneli za miale ya jua huko Cape town. Picha na RODGER BOSCH / AFP.
Mfanyakazi katika kiwanda cha kutengeneza paneli za miale ya jua huko Cape town. Picha na RODGER BOSCH / AFP.

Maafisa wa nchi za kiafrika na wajasirimali waliohudhuria mkutano mkuu wa Ujasirimali wa kimataifa na Afrika, wamesifu uwezekano mkubwa wa kuingia kwenye soko la Uchina na maendeleo ya haraka katika sekta ya nishati mbadala, ambayo wanaamini inatoa nafasi kubwa kwa nchi na biashara zao.

Mkutano huo na maonesho ya siku mbili yanayomalizika hii leo mjini Cape Town, Afrika Kusini umewaleta pamoja wajasiri mali na viongozi kutoka zaidi ya mataifa 50 ya Afrika ambao wanadhamira ya dhati kuimarisha kazi za ujasirimali kupitia nchi zao.

Moja wapo ya maendeleo makubwa ni kipindi cha kuelekea katika matumizi ya nishati safi inayotowa nafasi mpya kwa ajili ya biashara.

Kutokana na Afrika Kusini kukabiliwa na shida kubwa ya upungufu wa huduma za umeme, mjumbe Nakon Mengardi wa Afrika Kusini anasifu mbinu zinazotumiwa nba Uchina katika kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za jua, ikiwa njia moja wapo ya kuruhusu vbiwanda kuzalisha bidhaa zao wakati wa ukosefu wa umeme.

Forum

XS
SM
MD
LG