Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:05

Wanawake wa Kenya na Tanzania wakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji safi


Wanawake nchini Tanzania wakibeba maji
Wanawake nchini Tanzania wakibeba maji

Wanawake nchini Kenya na Tanzania ni miongoni mwa watu billioni mbili duniani wanaopitia changamato kubwa za ukosefu wa huduma za maji safi na salama ya kunywa, na pia ni miongoni mwa watu billioni 3.6 wasiokuwa na  huduma za usafi zinazosimamiwa kwa usalama.

Wakizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu katika siku ya maadhimisho ya maji duniani, wanawake wa eneo la Segerea lililopo katika jiji la Dar Es Salaam na Bombolulu, Kibera, nje ya jiji la la Nairobi, wanawake wamesema ukosefu wa maji safi na salama unaathiri shuguli zao za kila siku zikiwemo zile za kikazi, kibiashara na kifamilia.

Wamesema ukosefu wa maji katika meneo yao, unaleta changamoto nyingi kwa kuwa hutumia muda mwingi kufanya ‘mawindo’ ya maji ambayo husambazwa kwa mgao, nyakati za usiku katika meneo yao.

Violet Akinyi, mkazi wa Bombolulu, Kibira ameliiambia Sauti ya Amerika, tangu mwezi Januari, eneo lao limekuwa likipata maji kwa mgao ambayo husambazwa kwa muda mfupi mara mbili kwa wiki ambayo ni siku ya Ijumaa na Jumanne .

Amesema kiwango hicho cha maji huwa ni kidogo, hakitoshelezi mahitaji ya familia zao, kwa sababu wengi wao hawana uwezo wa kumudu pampu za kuongeza msukumo wa maji ambayo hutiririka kwa kasi ndogo.

Wameongeza kuwa maji hayo ya mgao unaodumu kwa kipindi cha kati ya masaa matatu au sita hayatoshi “kufua nguo za watoto za shule, na pia mgao huo unafanya tushindwe kutoa msaada wa maji kwa majirani.

Ukosefu wa maji katika maeneo yao umesababisha kuziba kwa vyoo na kuhatarisha milipoko ya majonjwa ya kipindupindu, Alisema Akinyi,

Naye Lucy Adongo, mmiliki wa biashara ya chakula, maarufu nchini Kenya kwa jina la ‘Kibadaski’ amesema ukosefu wa maji unaleta changamoto katika biashara yake ya upishi na uuzaji wa chakula, ambapo analazimika kununua maji machafu ya nvua yanayotoka kwenye mabwawa.

“Ninalazimika kununua na kutumia maji machafu kwa sababu nataka biashara yangu iendelee” Alisema Lucy.

Aliiambia Sauti ya Amerika kuwa mume wake haoigi kila siku, na ukosefu wa maji “unasababisha migogoro katika ndoa”

Kwa Tanzania tatizo la maji mara nyingi lipo katika meneo mapya na yale yaliyoko kando ya jiji la Dar es Salaam. Brigitte Sakumo mkazi wa Segerea, amesema mgao wa maji katika eneo lao unawafikia kila baada ya wiki mbili au mwezi mmoja.

“Changamoto hutokea “wakati unapoishiwa maji na huna pesa ya kuyanunua…tunanunua maji ya tangi lenye lita maji kwa shillingi 50,000,” aliongeza.

Kulingana na takwimu za mwaka 2020, asilimia 26 ya watu duniani (watu bilioni 2) hawakupata huduma ya maji ya kunywa iliyosimamiwa kwa usalama na inakadiriwa kwamba asili mia 46 (bilioni 3.6) hawakupata huduma iliyosimamiwa vyema ya usafi.

-Imetayarishwa na Mariam Kurtz, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG