Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:15

Maafisa wa Ukraine wanasema shambulizi la Drone limeuwa angalau watu watatu


Mfano wa maeneo yaliyoshambuliwa kwa Drone huko Kyiv, Ukraine.
Mfano wa maeneo yaliyoshambuliwa kwa Drone huko Kyiv, Ukraine.

Kitengo cha huduma ya dharura cha serikali kimesema shambulizi hilo lilipiga shule huko Rzhyshchiv, karibu kilomita 60 kusini mwa mji mkuu, na kuharibu majengo mawili ya wanafunzi na jengo la elimu

Maafisa wa Ukraine wamesema Jumatano kwamba shambulio la ndege isiyo na rubani (Drone) ya Russia usiku wa kuamkia Jumatano liliwaua watu wasiopungua watatu katika mkoa wa Kyiv.

Kitengo cha huduma ya dharura cha serikali kimesema shambulizi hilo lilipiga shule huko Rzhyshchiv, karibu kilomita 60 kusini mwa mji mkuu, na kuharibu majengo mawili ya wanafunzi na jengo la elimu. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ali-Twitt leo Jumatano kwamba mashambulizi ya Russia usiku wa kuamkia Jumatano yalijumuisha ndege 20 zisizo na rubani za Iran, pamoja na makombora.

Zelenskyy alisema kila wakati mtu anaposikia neno 'amani' huko Moscow, basi kuna amri nyingine hutolewa kwa mashambulizi kama hayo ya uhalifu,". Kiongozi huyo wa Ukraine amesema mafanikio ya vikosi vyake yanakaribia kuleta amani huku akitoa wito wa umoja wa kimataifa na kufuata vikwazo vinavyoilenga Russia.

XS
SM
MD
LG