“Wametengeneza hali ya taharuki” amesema Rabab, ambaye anaishi katika kijiji cha kaskazini mwa mji kuu wa jimbo la Wad Madani, Al-Jazira na eneo jipya lenye mapigano makali kati ya jeshi na vikosi vya Rapid Support Forces (RSF).
Kama wanavijiji wengine walioongea na AFP, Rahab ameomba atambuliwe kwa jina lake la mwanzo tu akihofia, kulipiziwa kisasi na wapiganaji ambao mara kwa mara wamekuwa wakiwalenga raia katika kipindi cha zaidi ya miezi minane ya vita.
Siku ya Jumamosi, watu wasiopungua wanane waliuawa na wapiganaji wa RSF katika kijiji kimoja kwenye jimbo la Al- Jazira, mashuhuda waliliambia shirika la habari la AFP kuwa walipigwa risasi baada ya kujaribu kuwazuai waporaji wao.
Kusini mwa Khartoum, watu zaidi ya nusu milioni wamejihifadhi huko Al- Jazira baada ya mapigano kuongezeka katika mji mkuu huo wa Sudan.
Hata hivyo, mwezi huu wanamgambo waliingia ndani zaidi katika jimbo na kuharibu moja ya maeneo matakatifu yaliyobaki, na kuwalazimisha zaidi ya watu 300,000 kukimbia kw amara nyingine tena, Umoja wa Mataifa umesema.
Wale waliobaki—hawawezi au hawataki kuondoka-- wamejikuta katika kile ambacho shirika la Msalaba Mwekundu unachokiita “mtego mwingine wa kifo”
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum