Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:51

Wananchi wapiga kura Jamhuri ya Afrika ya Kati wakipuuza vitisho vya waasi


Wapiga kura wajitokeza katika uchaguzi wa rais Jumapili katika kituo cha kupiga kura shule ya Barthelemy Boganda huko wilaya Bangui, Disemba 27, 2020. (Photo by ALEXIS HUGUET / AFP)
Wapiga kura wajitokeza katika uchaguzi wa rais Jumapili katika kituo cha kupiga kura shule ya Barthelemy Boganda huko wilaya Bangui, Disemba 27, 2020. (Photo by ALEXIS HUGUET / AFP)

Wapiga kura nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanapiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge Jumapili kama ilivyopangwa, wakipuuza vitisho vya ghasia vilivyotolewa na waasi.

Katika mji mkuu, Bangui mkazi wa mjini humo, Desire Ngaibona anasema : “Kwa kweli nimefurahi (kupiga kura) na nawataka raia, hata wale ambao bado wako majumbani, kujitokeza kupiga kura kwa wingi ili ifikapo kesho, amani irejee nchini mwetu.”

Mahakama ya Katiba imekataa ombi la upinzani Jumapili kuchelewesha uchaguzi huo.

Uchaguzi wa taifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati unafanyika wakati serikali, washirika wa kimataifa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameshirikiana kuzuia shambulizi lolote la waasi.

Rais Faustin Archange Touadera, ambaye anagombea awamu nyingine, anaonekana kuwa ndiye mgombea anayetakiwa kati ya wagombea wengine 17.

Touadera na wafuasi wake wamemshutumu kiongozi wa zamani, Francois Bozize, kwa kuwa upande wa waasi na kushawishi ghasia zinazolenga kuipindua serikali, shutuma ambazo Bozize amekanusha.

Hata hivyo, AFP imeripoti kuwa Jumapili Bozize aliwasihi watu kutopiga kura katika uchaguzi wa Jumapili.

Umoja wa Mataifa umemuwekea vikwazo Bozize na hivyo amezuiliwa kugombea katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huu.

XS
SM
MD
LG