Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:51

Wananchi wa Rwanda nchini Uganda waanza kupiga kura


Rais Paul Kagame akiwa katika kampeni Rwanda
Rais Paul Kagame akiwa katika kampeni Rwanda

Wananchi wa Rwanda wanaoishi Uganda Alhamisi walianza kupiga kura kwenye ubalozi wa Rwanda, Kampala.

Wamefika katika ubalozi huo ambao uko katika eneo la Kitante katika kitongoji cha mji wa Kampala, kumchagua mmoja kati ya wagombea watatu katika kinyang’anyiro cha urais.

Wanapiga kura siku moja mapema kabla ya siku ya uchaguzi wa urais iliyopangwa ambayo ni Ijumaa.

Rais aliyoko madarakani Paul Kagame, ambaye anapeperusha bendera ya chama cha Rwanda Patriotic Front ambacho alikiiongoza kushika madaraka, anatarajiwa kushinda kwa kura nyingi na yeye katika kampeni yake alitangaza kuwa uchaguzi “umemalizika” ikiwa sawa na kusema tayari amepata ushindi.

Upande wa upinzani wa chama cha Democratic Green party ambapo mgombea wake Frank Habineza na mgombea huru Philippe Mpayimana, ndio wapinzani pekee wa Kagame.

Wapiga kura wamejitokeza kutoka maeneo yote ya Uganda ambapo baadhi yao wamefika mapema sana alfajiri saa 3am.

Balozi wa Rwanda nchini Uganda Meja Jenerali Frank Mugambage ameeleza furaha yake kwamba wananchi wengi wa Rwanda wameshiriki katika zoezi hilo la kupiga kura.

XS
SM
MD
LG