Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:37

Wanaharakati hawaridhishwi na kasi ya WEF kuondoa umaskini


Takataka zinazokusanywa katika eneo la Dandora
Takataka zinazokusanywa katika eneo la Dandora

Eneo la Dandora la mabanda, makazi ya watu wa chini nchini Kenya ambapo mazingira ya uchafu yamekithiri na wiki hii ni sehemu ambayo wanaharakati wanakampeni dhidi ya umaskini.

Wanasema kuwa wamechoka na mazungumzo na wanaona hatua chache zinachukuliwa kutatua matatizo katika maeneo ambayo yameachwa nyuma na ni muhimu kuleta mabadiliko ya haraka.

Ni wakati ambapo mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika katika fukwe za hoteli ya Swiss Ski huko Davos linawaleta pamoja wanasiasa na mabilionea, makampuni makubwa na watu maarufu kwa siku nne ya mkutano huo juu ya masuala muhimu mno ya dunia – masuala kama ya ukosefu wa usawa duniani.

Lakini pamoja na kusheherekea mkutano wa 48 mwaka huu ambapo kila mwaka hufanyika, WEF imeshindwa kuzuia ongezeko la mwanya uliopo katika utajiri, wanaharakati wanasema, hivyo basi badala yake kushawishi mabadiliko katika matukio yao wenyewe yanayofanyika wakati WEF inakutana wiki hii.

“WEF imeendelea kuorodhesha kukosekana usawa kama ni moja ya changamoto kubwa za dunia, na WEF yenyewe inakiri kuwa bado hakuna unafuu wowote.

Lakini pia hawana nia ya kutatua tatizo hili,” anasema Ben Phillips, mkurugenzi wa taasisi ya Global Inequality Alliance inayopigania usawa duniani, ambayo ni muungano wa taasisi 150 za hisani na vyama vya wafanyakazi katika nchi 50.

Phillips amesema jamii katika nchi hizi kama vile Kenya, Afrika Kusini, India, Pakistan, Indonesia na Mexico wanahisi kuwa ukosefu wa usawa hauwezi kuondolewa na ‘mtu wa Davos’ lakini na watu wenyewe kwa kuhamasishana kupigania haki zao.

Kwa hiyo kutakuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo maonyesho na mashindano ya soka, vyakula na maandamano—yatafanyika ili kusaidia baadhi ya maeneo yaliyokuwa yameathiriwa na umaskini kujua haki zao na kushinikiza kuchukuliwa hatua kutatua matatizo yao.

Eneo hilo duni la Dandora ambalo liko nje kidogo mashariki mwa Nairobi ni mfano halisi wa kukosekana usawa kunakowakabili mamilioni ya watu duniani.

Lilianzishwa mwaka 1977 na kufadhiliwa kwa kiasi fulani na Benki ya Dunia, ikiwa na lengo la kusaidia kuwepo makazi bora lakini hivi leo eneo hilo limekuwa ni eneo lenye jaa kubwa la kutupa uchafu.

XS
SM
MD
LG