Shule hiyo ilifungwa kwa muda na Waziri wa Elimu Fred Matiang’i baada ya bweni kuteketea kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi 9.
Wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wamefuatana na wazazi wao. Wazazi na wanafunzi walipewa ushauri nasaha kabla ya ibada maalum kufanyika shuleni hapo.
Wanafunzi ambao walihojiwa na vyombo vya habari wamesema kwamba bado wameathirika kisaikolojia na tukio hilo lakini wamesema wamefarijika na hatua zilizochukuliwa na shule hiyo kutafuta ufumbuzi wa kero zilizoelezwa na wanafunzi na wazazi.
Kwa upande wao wazazi wamesema kuwa ushauri nasaha uliotolewa ni wenye weledi wa kutosha.
Wamesema kuwa shule imewahakikishia kuwa zoezi hilo la kuendelea kuwapa moyo wanafunzi ili kuondokana na hofu iliyotokana na moto huo litaendelea.
Kama wazazi tunaimani kuwa wanafunzi wako katika mazingira salama, alisema mmoja wa wazazi waliokuja na watoto wao John Mwangi akiwa na mkewe Nancy,
Wanafunzi walikuwa wamejawa na matumaini japokuwa bado wanahofu. Na ndio maana watoa ushauri nasaha wapo hapa kwa ajili ya kuwasaidia, taarifa ya shule ilieleza hivyo.