Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:06

Uganda yawachunguza wanadiplomasia wa China


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Serikali ya uganda inawachunguza maafisa wa ngazi ya juu katika ubalozi wa china nchini Uganda, kwa kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu.

Wanadiplomasia hawa wanachunguzwa kwa kushirikiana na maafisa katika hifadhi za wanyama pori katika nchi za Uganda, Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan katika kufanya biashara hiyo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa barua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, imeamrisha uchunguzi wa kina dhidi ya ubalozi wa china nchini humo, pamoja na kiongozi mkuu wa mamlaka ya hifadhi ya wanyama pori.

Uchunguzi huo unafuatia madai yakuwa watu wote hao wanahusika katika biashara haramu ya wanyama wa mwituni, na pembe za ndovu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:58 0:00

Wanadiplomasia Li Wejin na Yinzhi katika ubalozi wa China nchini Uganda, wanadaiwa kuwa wafanyabiashara wakuu wa pembe za ndovu katika nchi za Afrika Mashariki na maziwa makuu, hadi Afrika ya Kati.

Kando na kufanya biashara hiyo kati ya Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Afrika ya Kati na Sudan Kusini, wanadiplomasia hao wanaripotiwa kushirikiana na maafisa wakuu nchini Uganda na kuiba pembe za ndovu zenye uzito wa kilo 1300, thamani ya shilingi bilioni 3 pesa za Uganda.

Kulingana na washikadau katika sekta ya utalii wanaomba kutotajwa majina, biashara hiyo haramu imekuwa ikifanyika kwa miaka zaidi ya 10 sasa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Uganda

XS
SM
MD
LG