Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:47

Wanachama wa Kamati ya Olimpiki, IOC, wamtaka rais wake kuendelea kuongoza kwa muhula wa tatu


Mkutano wa IOC nchini India
Mkutano wa IOC nchini India

Wanachama kadhaa wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki walitoa wito Jumapili kwa Rais Thomas Bach kusalia katika wadhifa huo baada ya muhula wake wa pili kumalizika mwaka 2025 na kuendelea kwa muhula  wa tatu, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Bach alichaguliwa mwaka wa 2013, na anatarajiwa kuachia nafasi hiyo mwaka 2025 kwa mujibu wa kanuni za sasa za Olimpiki, kufuatia muhula wa kwanza wa miaka minane na wa pili wa miaka minne.

IOC, hata hivyo, ilisema itajadili suala hilo katika mkutano ujao wa bodi kuu.

Tamko la wazi la Jumapili la wanachama wa IOC lilifuatia uvumi katika miezi ya hivi karibuni kwamba Bach anaweza kuendelea kama rais wa moja ya mashirika yenye nguvu zaidi katika michezo ya kimataifa.

Kufikia sasa hakuna mwanachama wa IOC ambaye ametangaza nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu, ingawa kuna watu kadhaa wanaoonekana kama wanaweza kujitosa uwanjani.

Idadi ya mihula hiyo ilipunguzwa ili kuepusha uwezekano wa kukaa uongozini kwa muda mrefu kama vile rais wa zamani Juan Antonio Samaranch, ambaye aliongoza kwa miaka 21 kutoka 1980 hadi 2001.

Forum

XS
SM
MD
LG