Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:08

Ukraine yasema mashambulizi zaidi yaua watu, huku IOC ikipinga madai ya Ukraine


Picha ya Maktaba: Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy.
Picha ya Maktaba: Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy.

Ukraine, Jumatatu imesema kwamba mashambulizi ya Russia yameua raia watano zaidi, na kujeruhi wengine 13 katika kipindi cha saa 24, lakini pande hizo mbili hazijapata mafanikio zaidi katika mapambano makali mashariki mwa Ukraine.

Serekali imesema vifo vinajumuisha mwanamke ambaye aliuwawa, na wengine watatu walijeruhiwa katika mashambulizi ya Russia katika wa kasakzini mashariki wa Kharkiv, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa.

Vikosi vya Russia vilishikilia sehemu nyingi za mkoa wa Kharkiv, kwa sehemu kubwa ya vita vya mwaka mmoja, lakini mashambulizi ya majibu ya Ukraine yaliwezesha kupata udhibiti mwezi Agosti mwaka jana.

Mashambulizi ya Ukraine na Russia katika mji wa kusini wa Ukraine wa Kherson na kuua watu watatu Jumapili na wengine sita kujeruhiwa.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema majengo ya makazi, hospitali, shule, vituo vya mabasi, posta na benki zilishambuliwa.

Wakati huohuo kamati ya kimataifa ya Olympic, Jumatatu imepinga ukosoaji unaotolewa na maafisa wa Ukraine, ambao wameshutumu kwa kuunga mkono vita baada ya taasisi hiyo kusema kwamba kuna uwezekano Russia inaweza kupewa fursa ya kufuzu michezo ya olimpiki ya Paris, 2024.

Mshauri wa rais wa Ukraine, Mykhailo Podolyak mwishoni mwa juma alielezea kwamba IOC inachochea ghasia, mauaji ya wengi, usumbufu, na Jumatatu alieleza pia kwamba uwepo wa Russia kwenye michezo hiyo kutaipa nchi hiyo ya kuendeleza mauaji ya kimbari.

Mapema Jumatatu, waziri wa mambo ya nje Dmytro Kuleba alitoa wasiwasi wa ukweli kwamba wanamichezo wengi wa Russia walikuwa na ushirikiano na jeshi, ikijumuisha kushiriki kwa michezo ya vilabu yenye ushirikiano na wizara ya ulinzi.

Russia imepinga shutuma hizo kwamba vikosi vyake vimefanya unyama nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG