Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:56

Walibya waandamana kupinga "mamlaka kukosa uwajibikaji" kuhusiana na mafuriko


Mafuriko nchini Libya
Mafuriko nchini Libya

Mamia ya watu waliandamana Jumatano katika mji wa mashariki mwa Libya wa Derna, kuelezea ghadhabu yao kwa kile walichodai ni mamlaka kukosa uwajibikaji, wiki moja baada ya mafuriko kuua maelfu ya wakazi wake na kusababisha uharibifu mkubwa.

Waandamanaji hao walilenga maafisa, akiwemo mkuu wa bunge la Libya lenye makao yake mashariki mwa nchi, Aguila Saleh, walipokusanyika nje ya Msikiti wa Sahaba.

Wengine waliketi juu ya paa la jengoi la jengo la bunge, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Baadaye jioni, waandamanaji wenye hasira walichoma moto nyumba ya aliyekuwa meya wa mji wa Derna wakati wa mafuriko hayo, Abdulmenam al-Ghaithi, meneja wa ofisi yake aliliambia shirika la habari la Reuters.

Reuters haikuweza mara moja kumfikia Ghaithi kwa maoni yake.

Maandamano ya Jumatatu ndiyo ya kwanza tangu mafuriko hayo, ambayo ambayo yalibebe vitongozi vizima, hasa baada ya mabwawa mawili kuvunja kingo katika moja ya mikasa mibaya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG