Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:10

Waislamu washerehekea Sikukuu ya Eid huku mapigano Sudan yakiendelea


Waislamu waadhimisha Eid Al-Fitr
Waislamu waadhimisha Eid Al-Fitr

Waislamu nchini Kenya na  kwingineko  duniani wamekamilisha mfungo wa mwezi wa ramadhani na kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri kwa sala. Lakini sherehe hizi zimegubikwa na mapigano yanayoendelea ya kuidhibiti sudan na tukio la mkanyagano lililosababisha vifo nchini Yemen.

Kalenda ya kiislamu inafuata kuandama kwa mwezi ambapo mara nyingine viongozi wa dini ya kiislamu wanapingana nayo.

Sherehe za Eid El Fitri zinafanyika baada ya waumini wa kiislamu kufunga mwezi wa ramadhani kuania alfajiri hadi jua linapotua wakati wa jioni.

Kwa mara nyingine tena mwaka huu sherehe hizi zinakuja wakati ambapo kuna mapigano na hali ya kutaabika hasa huko Mashariki ya Kati.

Nchini Sudan, sherehe hizi zimegubikwa na mapigano baina ya jeshi na kundi hasimu la kijeshi, licha majaribio mawili ya sitisho la mapigano.

Huko Yemen taifa maskini sana katika dunia ya kiarabu, jumatano lilishuhudia mkanyagano wakati wa tukio la hisani la kuwapatia msaada wa fedha watu katika eneo linalodhibitiwa na waasi- Sanaa na kusababisha vifo vya watu 78 na kujeruhi wengine 77.

XS
SM
MD
LG