Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 16:45

Wahome kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake


Dereva wa magari ya mashindano Maxine Wahome (kulia) na wakili wake Cliff Ombeta, wakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu Nairobi, Januari 12, 2023. Picha na Tony KARUMBA / AFP.
Dereva wa magari ya mashindano Maxine Wahome (kulia) na wakili wake Cliff Ombeta, wakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu Nairobi, Januari 12, 2023. Picha na Tony KARUMBA / AFP.

Dereva wa mbio za magari nchini Kenya Maxine Wahome Jumatano alishtakiwa kwa kosa la kumuua mpenzi wake, siku moja baada ya kuonekana kuwa katika hali nzuri kujibu mashtaka.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 26 alikana shtaka hilo wakati alipoonekana kwenye video ya mahakama kuu iliyoko katika mji mkuu wa Nairobi.

Wahome anatuhumiwa kumshambulia mpenzi wake Asad Khan mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni dereva, wakiwa kwenye nyumba yao mwezi Desemba mwaka jana.

Khan alifariki dunia kutokana na majeraha kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia baada ya kulazwa hospitali kwa wiki moja.

"Sina hatia," Wahome aliiambia mahakama.

Wahome alipata sifa kubwa akiwa mwanamke wa kwanza Mkenya kushinda mbio za magari za daraja la tatu za WRC Safari Rally mwaka jana. Wiki iliyopita, Wahome aliondolewa kwenye programu ya WRC Young Rally Stars.

Katika nyaraka za mahakama ambazo Shirika la bahari la AFP imeziona, Wahome alisema Khan alijiumiza baada ya kupiga teke mlango wa kuelekea barazani ambao aliutumia kujihami baada ya kupigana naye.

"Marehemu alijijeruhi kwenye vioo vya dirisha na baadaye alikwenda hospitali," alisema.

Hakimu aliamuru mtuhumiwa abaki rumande hadi Machi 21 wakati ombi lake la dhamana litakaposikilizwa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG