Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:57

Wahanga wa mafuriko Kinshasa wafikia 44


Mafuriko na maporomoko yameuwawatu 44 katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jiji la tatu kwa ukubwa Afrika, afisa mmoja amesema Ijumaa.

“Tuna idadi ya vifo ya mwisho ambayo inaonyesha watu 44 wamekufa,” amesema waziri wa afya na masuala ya jamii wa jimbo hilo, Dominique Weloli. Idadi ya awali ya waliopoteza maisha ilikuwa ni watu 37.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP robo tatu ya makazi ya wananchi wa Kinshasa ni vibanda ambavyo havina mfumo maji taka wala umeme, kwa mujibu wa aliyekuwa mkuu wa shirika la UN-Habitat, Corneille Kanene.

Mvua kubwa na maporomoko yaliyotokea usiku kucha Jumatano yaliharibu nyumba hizo ambazo zilikuwa zimejengwa pembeni ya mlima.

Kinshasa ambayo ni makazi ya watu takriban milioni 10, ni jiji la tatu lenye watu wengi Afrika baada ya Cairo na Lagos.

XS
SM
MD
LG