Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:30

Watu 37 wafariki kutokana na mafuriko Kinshasa


Magari yaliyozama ndani ya maji kutokana na mafuriko jijini Kinshasa, Januari 4 2017. (VOA/TopCongo)
Magari yaliyozama ndani ya maji kutokana na mafuriko jijini Kinshasa, Januari 4 2017. (VOA/TopCongo)

Waziri wa huduma za jamii wa jimbo la Kinshasa, Dominique Weloli, anasema wanatarajia idadi ya walofariki kuongezeka baada ya mvua nyingi za siku kadhaa kusababisha maafa katika jimbo lao.

Wilaya 10 kati ya 24 za mji mkuu wa Kinshasa hazina huduma ya umeme kutokana na kwamba kituo kimoja muhimu cha umeme cha Kampuni ya Taifa ya Umeme kimefunikwa na maji ya mvua nyingi iliyonyesha Jumatano usiku kuamkia Alhamisi.

Kituo kikuu cha umeme cha Kinshasa kimeja maji ya mvua Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
Kituo kikuu cha umeme cha Kinshasa kimeja maji ya mvua Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)

Maafisa wanasema baadhi ya nyumbe zimeporomoka na mmomonyoko wa ardhi umesababisha maafa katika maeneo mengine.

Wakazi wengi wa jiji hilo wanawalaumu maafisa wa serikali kwa kutoshughulikia miundo mbinu hasa mitaro iliyojaa takataka na kusababisha mafuriko hayo.

Kinshasa ni moja wapo ya miji ya Afrika yenye wakazi wengi, inakadiriwa kuna wakazi milioni 10 katika jiji hilo na vitongoji vyake wengi wakiishi katika hali duni ya maisha.

XS
SM
MD
LG