Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:59

Wagner yadaiwa kuisaidia RSF Sudan


Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) kikiwa katika wilaya ya Nile huko Khartoum, tarehe 23 Aprili 2023. Picha na RSF) / AFP.
Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) kikiwa katika wilaya ya Nile huko Khartoum, tarehe 23 Aprili 2023. Picha na RSF) / AFP.

Yevgeny Prigozhin ni mkuu wa kundi la kijeshi linaloungwa mkono na Russia, ametoa silaha kwa moja ya pande zinazopigana nchini Sudan, kulingana na ripoti kadhaa za vyombo vya habari.

Tangu mapigano yalipoanza mwezi Aprili, kumekuwa na ripoti ambazo hazijathibitishwa, na vyanzo vya kidiplomasia ambavyo vilizungumza na vyombo vya habari vilisema kwamba wapiganaji wa Wagner wanaliunga mkono na kulipatia silaha kundi la wanamgambo linalojulikana kama Rapid Support Forces.

Afisa wa zamani wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na mshirika mwandamizi katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa, Cameron Hudson, aliiambia Sauti ya Amerika kuwa Kundi la Wagner linatoa mifumo ya ulinzi wa anga, roketi, vifaru na silaha nzito za kivita.

RSF imekanusha kupokea msaada kutoka Russia.

Wakati habari zinaibuka, hata hivyo, kwamba Kundi la Wagner linaweza kuwa linauunga mkono upande mmoja wa mapigano, wataalam wanaonya kujihusisha kwa kundi hilo la nje inaweza tu kuuzidisha mzozo huo, wakitoa mfano wa rekodi mbaya ya kundi hilo lenye mlolongo wa vitendo vya ukatili barani Afrika.

Kwa nadra kundi hilo limekuwa likikiri kuhusika nchini Sudan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov alisema Jumanne kwamba uamuzi wa kulihusisha Kundi la Wagner ni juu ya uongozi wa Afrika.

"Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mali na Sudan, na nchi kadhaa nyingine ambazo serikali zake zina mamlaka halali kwa huduma za aina hii [kwa Wagner Group], na zina haki ya kufanya hivyo," Lavrov aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa.

Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani wanaendelea kuelezea wasiwasi wao kuhusu kuhusika kwa Kundi la Wagner nchini Sudan, ambako linajihusisha na uchimbaji madini.

XS
SM
MD
LG