Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:26

Waendesha mashtaka nchini DRC waomba adhabu ya kifo dhidi ya washtakiwa 50 katika kesi ya jaribio la mapinduzi


Washtakiwa wa jaribio la mapinduzi nchini DRC wakiwa mahakamani mjini Kinshasa, Juni 7, 2024. Picha ya AP
Washtakiwa wa jaribio la mapinduzi nchini DRC wakiwa mahakamani mjini Kinshasa, Juni 7, 2024. Picha ya AP

Waendesha mashtaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumanne waliomba washtakiwa 50 kufikishwa mahakamani na kukabiliwa na adhabu ya kifo kutokana na kile jeshi linasema ni kushiriki katika jaribio la mapinduzi.

Miongoni mwa washtakiwa hao kuna raia watatu wa Marekani.

Mwendesha mashtaka wa jeshi Luteni Kanali Innocent Radjabu amewataka majaji kuwahukumu kifo wale wote wanaokabiliwa na kesi ya jaribio la mapinduzi la mwezi Mei, isipokuwa mshtakiwa mmoja.

Watu wenye silaha walishambulia nyumba ya waziri wa Uchumi Vital Kamerhe mapema asubuhi tarehe 19 Mei, ambaye alichaguliwa kuwa spika wa bunge la taifa siku tatu baadaye.

Kundi hilo baadaye lilijielekeza ikulu ambako kuna ofisi za Rais Felix Tshisekedi, likipeperusha bendera za Zaire, jina la nchi hiyo chini ya kiongozi wa zamani Mobutu Seseko aliyeondolewa madarakani mwaka 1997.

Jaribio hilo la mapinduzi lilikuwa linaongozwa na Christian Malanga, raia wa Congo ambaye alipata uraia wa Marekani na ambaye aliuawa na maafisa wa usalama, msemaji wa jeshi Sylvain Ekenge alisema wakati huo.

Wakati wa kuhojiwa, washtakiwa waliokamatwa walimlaumu Malanga.

Richard Bondo, ambaye anamtetea mmoja wa washtakiwa raia wa Marekani, aliiambia AFP kwamba adhabu ya kifo iliyoombwa na waendesha mashtaka ni “kali sana.”

Forum

XS
SM
MD
LG