Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:40

Wabunge wamwambia Museveni kubadilisha katiba ni sumu


Rais Yoweri Kaguta Museveni
Rais Yoweri Kaguta Museveni

Hatua ya serikali ya Uganda kutaka kubadilisha katiba ili iwe na nguvu za kumiliki ardhi mahali popote wakati wowote, imepata pigo baada ya wabunge wa chama tawala kukataa kumuunga mkono rais Museveni.

Wabunge wamemueleza Museveni kwamba hatua yake ya kutaka kubadilisha katiba ni sumu kwa taifa.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ameripoti kuwa wabunge hao 278 kutoka chama tawala cha national resistence movement NRM, walikataa nia ya serikali kutaka kuifanyia katiba marekebisho, katika mkutano ulioitishwa Alhamisi na Rais Museveni katika ikulu ya rais ya Entebbe, karibu na jiji la Kampala.

Wabunge, wamemweleza rais Museveni kwamba hakuna namna angeweza kuwashawishi raia kukubali kuifanyia katiba marekebisho ili kuiruhusu serikali kumiliki ardhi kimabavu, wakati wowote, pahali popote, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali.

Wabunge, wametaja hatua hiyo kuwa sumu kwa taifa kwani raia wana imani kwamba serikali inataka kuwaibia ardhi.

Ruth Nankabirwa, ni kiranja wa serikali bungeni amesema : “Msimamo ni kwamba hamna haja ya kubadilisha ibara 26 ya katiba. Tumekubaliaan kuunda kamati maalum kuhusu ardhi ili kuhakikisha kwamba miradi ya serikali inatekelezwa kwa wakati, wanaomiliki ardhi hawanyanyaswi.

Badala yake, wabunge hao wamekubaliana kuunda kamati maalum itakayokuwa ikishughulikia maswala ya ardhi kote nchini, endapo serikali inataka kutekeleza miradi ya maendeleo mahali popote pale.

Kamati hiyo, itakuwa na mda wa siku 90 kukamilisha vikao vyake, na iwapo mwenye ardhi hajaridhika, atalazimika kwenda mahakama kuu itakayosikiliza kesi kwa muda usiozidi siku 3, huku baadhi ya wabunge wakiunga mkono vitendo vya kuchoma greda zinazotumika katika uvamizi wa ardhi.

Suala kuu ni kuhakikisha kwamba miradi ya serikali inatekelezwa kwa muda ili kuhakikisha waganda hawapati hasara. Wabunge wote waliohudhuria kikao wamekubaliana kwamba ni lazima miradi ya serikali itekelezwe.

Na baada ya wabunge kukataa pendekezo la Museveni kutaka ibara ya 26 ya katiba kufanyiwa marekebisho, mmoja wa wabunge waliohudhuria kikao hicho amearifu sauti ya amerika kwamba museveni amemalizia kikao kwa msemo kwamba rangi yap aka haijalishi, ilimradi paka huyo anaweza kumshika panya.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennes Bwire, Uganda

XS
SM
MD
LG