Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:51

Wabunge wa Marekani wapitisha mswada ambao unaweza kusabisha marufuku kwa TikTok


Nembo ya TikTok
Nembo ya TikTok

Mtandao wa TikTok kwa mara nyingine umejikuta katika hali tete baada ya wabunge wa Marekani kupitisha mswada ambao utapelekea mtandao huo kupigwa marufuku nchini kote Marekani.

Baraza la Wawakilishi Jumatano lilipitisha mswada ambao utaipiga TikTok marufuku ikiwa mmliki wake mwenye makao yake China, ByteDance hatauza hisa zake katika mtandao huo maarufu wa kijamii ndani ya miezi sita mswada huo ukisainiwa kuwa sheria.

Ikiwa ByteDance itaamua kuuza hisa zake, TikTok itaendelea kufanya kazi nchini Marekani, ikiwa Rais atabaini “kupitia mchakato wa idara tofauti” kwamba mtandao huo “haudhibitiwi tena na adui wa kigeni.

Wataalam walisema itakuwa changamoto kwa ByteDance kuiuza TikTok katika miezi michache.

Ikiwa kampuni hiyo itakata kuuza hisa zake, TikTok itapigwa marufuku kutumiwa kwenye app za Apple na Google, vile vile kwenye huduma nyingine za mtandaoni hadi uuzaji huo utakuwa umefanyika, kulingana na mswada huo.

Wabunge kutoka vyama vyote, vile vile maafisa wa usalama na ujasusi, walielezea wasiwasi wao kwa muda mrefu kwamba mamlaka za China zinaweza kuilazimisha ByteDance kukabithi taarifa za Wamarekani milioni 170 wanaotumia TikTok.

Forum

XS
SM
MD
LG