Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 22:50

Wabunge Somalia wakubaliana kuongeza muda wa kufanyika uchaguzi


Mlipuko uliotokea Mogadiscio, Somalia, Februari 16, 2022. (AP foto/Farah Abdi Warsameh)
Image
Mlipuko uliotokea Mogadiscio, Somalia, Februari 16, 2022. (AP foto/Farah Abdi Warsameh) Image

Wabunge wa Somalia wamekubaliana kuongeza muda wa uchaguzi wa wabunge hadi Machi 15 katika uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu.

Serikali iliweka tarehe ya mwisho kwa uchaguzi wa bunge kukamilika Ijumaa.

Ofisi ya Waziri Mkuu imesema katika taarifa yake kuwa wabunge wameshindwa kufikia tarehe hiyo kwa sababu ya ukosefu wa fedha na usalama.

Uchaguzi wa bunge umeanza Novemba kuchagua wabunge ambao baadae watamchagua rais mpya.

Hadi hivi sasa ni theluthi mbili ya viti 275 vya wabunge ambavyo vimezibwa.

Somalia inajitahidi kuujenga tena uchumi wake baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Somali ilishindwa kufanya uchaguzi mwezi Februari mwaka 2021, na badala yake wabunge waliongeza muda wa Rais Mohamed Abdulahi kubaki madarakani.

XS
SM
MD
LG