Polisi wanasema kuwa takriban watu 15 wamefariki dunia baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kutegua milipuko katika fulana ya aliyokuwa amevaa kwenye mgahawa uliojaa watu wakati wa chakula cha mchana huko Beledweyne, mji mkuu wa mkoa wa Hiran nchini Somalia.
Waliofariki wengi wao walikuwa raia, na watu wengine 20 walijeruhiwa, msemaji wa polisi Dini Roble Ahmed aliliambia Shirika la habari la Associated Press kwa njia ya simu.
Mlipuko huo ulisababisha uharibifu mkubwa, alisema.
Kundi lenye itikadi kali la al-Shabab lilidai kuhusika.
Mlipuko huo unakuja huku kukiwa na mchakato wa uchaguzi wa Somalia uliocheleweshwa kwa muda mrefu na mara nyingi mchakato wenye mvutano.