Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:05

Vyama vya Upinzani kufufua mchakato wa kutokuwa na imani na Ramaphosa


Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini imesema Alhamisi kuwa mwezi ujao itasikiliza kesi iliowasilishwa na vyama viwili vya upinzani ikilenga kufufua mchakato wa kutokuwa na imani na Rais Cyril Ramaphosa.

Hatua hiyyo ni kufuatia kashfa ya zaidi ya dola laki 5 taslimu zilizopatikana kwenye nyumba moja shambani mwake na kisha kuibiwa. Ramaphosa aliponea kura hiyo mwaka 2022 baada ya chama chake cha ANC kutumia wingi wake bungeni kuipinga, hata baada ya ripoti ya uchunguzi huru kuhoji tabia yake na kupendekeza uchunguzi zaidi ufanywe.

Tangu wakati huo ANC kimeungana na vyama vingine 9, katika kuunda serikali ya muungano, hatua ambayo imetuliza malalamishi dhidi ya Ramaphosa kutokana na kashfa hiyo. Hata hivyo vyama viwili ambavyo siyo sehemu ya muungano huo, vya Economic Forum Fighters, na African Transformation Movement viliwasilisha kesi hiyo, vikidai kuwa bunge halikutekeleza kujumu lake la kikatiba la kuwajibisha Rais.

Kashfa hiyo ilizuka Juni 2022, na kutishia utawala wa Ramaphosa. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71 alichaguliwa tena Juni kwa muhula wa pili kupitia usaidizi wa wabunge wa upinzani baada ya chama chake cha ANC kupoteza wingi wake bungeni kwa mara ya kwanza tangu Afrika Kusini ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wabeberu mwaka 1994.

Forum

XS
SM
MD
LG