Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:42

Volcano yauwa zaidi ya watu 25 Guatemala


Mlipuko wa volcano nchini Guatemala
Mlipuko wa volcano nchini Guatemala

Idara ya kusimamia majanga nchini Guatemala imesema kuwa watu wasiopungua 25 wamepoteza maisha baada ya volcano kulipuka Jumapili karibu na mji wa Guatemala, na rojo lenye moto kutawanyika katika vijiji vya karibu na kuvifunika kwa moshi na majivu.

Volcano hiyo inayojulikana kama “volcano ya moto” huko Guatemala iliripuka kabla ya saa sita mchana.

Maafisa wanaosimamia majanga wamesema idadi ya watu isiyojulikana hawajulikani walipo, wakati zaidi ya watu 3,000 walihamishwa kutoka katika jamii za karibu na zaidi ya watu 600 wamewekwa katika kambi za muda huko katika majimbo ya Escuintla na Sacatepequez.

Vyombo vya usalama vimesema kuwa watu wanne waliuwawa katika kijiji cha El Rodeo wakati rojo hilo lenye moto ilipoangamiza nyumba hiyo, na watoto wawili wakauwawa kwa kuchomeka wakiwa katika daraja wanashuhudia mlipuko huo wa volcano.

Fuego iko takriban kilomita 44 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala na ambao uko karibu na mji wa Antigua, ambacho ni eneo linalopendwa sana na watalii.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa La Aurora ulifungwa kwa sababu ya tishio la jivu la moto la volcano hiyo kwa ndege zinazoruka angani.

XS
SM
MD
LG