Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 18:07

Viongozi wa Pasifiki wakutana Tonga


Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese
Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese

Viongozi wa mataifa ya Pasifiki walifanya mkutano wao wa kila mwaka huko Nuku’alofa Tonga leo Jumatano, huku Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese akipata uungwaji mkono wa kikanda kwa Mpango wa usalama wa Pasifiki.

Albanese aliwaambia waandishi wa habari katika Mkutano huo wa Visiwa vya Pasifiki kwamba uidhinishaji wa mpango huo ulikuwa lengo kuu la kikao hicho na kwamba utaimarisha usalama katika eneo hilo.

Waziri mkuu wa Tonga na mwenyekiti wa jukwaa anayekuja Siaosi Sovaleni alikaribisha makubaliano hayo.

Pacific Policing Initiative (PPI) ina nguzo tatu; Hadi vituo vinne vya mafunzo ya polisi vya kikanda vilivyo katika Pasifiki; Kikundi cha Msaada wa Polisi cha Pasifiki (PPSG), uwezo wa polisi wa nchi nyingi; na Kituo cha Maendeleo cha maafisa wa usalama na Uratibu cha PPI kitakachokuwa huko Brisbane, Albanese ilisema katika taarifa.

Kuna zaidi ya wajumbe 1,500 kutoka zaidi ya nchi 40 katika mkutano wa mwaka huu wa nchi wanachama wa Pasifiki, wote wakiwa na matumaini ya kuendeleza ajenda zao katika eneo ambalo bahari, rasilimali na nguvu za kimkakati zimekua zikibishaniwa

Forum

XS
SM
MD
LG