Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese Jumatatu aliikosoa China kwa hatari kubwa ya kukutana kati ya meli za kivita za China na Australia lakini alikataa kusema ikiwa amelielezea katika mazungumzo ya hivi karibuni na Rais Xi Jinping.
Alisema mpiga mbizi mmoja wa Australia alijeruhiwa wakati meli ya kichina ilipotumia darubini wakati ikiwa karibu na meli ya kivita ya Australia katika maji ya kimataifa Jumanne iliyopita.
Waziri wa ulinzi Richard Marles alisema Jumamosi kuwa ameelezea wasiwasi wake mkubwa kwa Beijing kuhusu uharibifu usio salama na tabia hiyo isiyo ya kitaalamu. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China, Wu Qian amepuuza madai ya Australia akisema hayana ukweli wowote.
Kati ya mkutano huo na taarifa ya Marles, Albanese alizungumza na Xi pembeni mwa mkutano wa viongozi wa Asia na Pasifiki huko San Francisco nchini Marekani.
Forum