Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:10

Marekani inaimarisha ushirikiano wake na China


Waziri wa mambo ya Nje wa China, Qin Gang (L) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken. Picha hii imetengenezwa June 13, 2023
Waziri wa mambo ya Nje wa China, Qin Gang (L) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken. Picha hii imetengenezwa June 13, 2023

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza Jumatano kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken atasafiri kwenda Beijing wiki hii na anatarajiwa kukutana na maafisa waandamizi wa China akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema

Marekani inaimarisha ushirikiano na China wakati ikiona uwezekano wa kupotoshwa ukiongezeka kwa mshindani wake wa juu, maafisa wa Marekani wamesema.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imetangaza Jumatano kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken atasafiri kwenda Beijing wiki hii. Wakati wa ziara hiyo, Blinken anatarajiwa kukutana na maafisa waandamizi wa China, akiwemo waziri wa mambo ya nje wa China, Qin Gang, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

Ziara hiyo inaonekana kama sehemu ya juhudi za utawala wa Biden kurekebisha uhusiano na Beijing baada ya mfululizo wa majibizano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Tunakuja Beijing na njia ya kweli, ya ujasiri na nia ya dhati ya kusimamia ushindani wetu kwa njia ya uwajibikaji zaidi iwezekanavyo, alisema Daniel Kritenbrink, waziri mdogo wa mambo ya Asia Mashariki na Pasifiki, alizungumza kwa njia ya simu katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG