Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 01:34

Viongozi wa nchi za pembe ya Afrika wakutana Eritrea


Viongozi wa Misri, Somalia na Eritrea wakutana Eritrea October 10, 2024. Pichna na AFP
Viongozi wa Misri, Somalia na Eritrea wakutana Eritrea October 10, 2024. Pichna na AFP

Viongozi wa Misri, Eritrea na Somalia wamekutana siku ya Alhamis katika mji wa Asmara, ambao ni mji mkuu wa Eritrea wakati kukiwepo na ongezeko la mvutano katika kanda ya pembe mwa afrika.

Wasi wasi kuhusu Usalama na uthabati katika kanda hiyo umeongezeka tangu Ethiopia kutia saini mwezi Januari mkataba wenye utata na jimbo lililojitenga la Somaliland, ili kuweza kupata njia ya kutumia bandari zake.

Mkataba huo wa ushirikiano wa usafiri wa baharini uliikasirisha Mogadishu na kuongeza uhasama wa kikanda wakati uhusiano ulizidi kuwa mbaya kati ya mataifa hayo jirani ya Ethopia na Somalai pamoja na Misri.

Marais Isaias Afwerki wa Eritrea, Abdel Fatah al sisi wa Misri na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia walikutana katika mji huo wa asmnara kufuatana na ujumbe kwenye ukurasa wa X wa ofisi ya rais Moghamud.

Wizara ya habari ya Eritrea imesema kwamba viongozi hao wamezingatia zaidi juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo tatu pamoja na kuzungumzia masuala ya usalama na utulivu katika kanda ya pembe mwa afrika.

Mohamud ambae ameshatembelea Eritrea mara kadhaa mwaka huu alikuwa na mazungumzo ya kando na mwenzake Jumatano jioni mara baada ya kuwasili.

Walijadili hasa juu ya kuimarisha ushirikiano na jukumu kubwa linalowakabili katika kulinda uhuru umoja na mipaka ya Somalia.

Al Sisi ambaye anaungana mkono na Somalia kwenye ugomvi huu aliwasili Asmara siku ya Alhamis kwa mazungumzo hayo ya pande tatu ikiwa ni nziara yake ya kwanza nchini humo.

Makubaliano ya muelewano kati ya Addis Ababa na Hargesa Somaliland ni ya kuiwezesha Ethiopia moja wapo ya mataifa makubwa yasio na mpaka na bahari dunaini kukodi sehemu ya pwani ya Somaliland kwa ajili ya kujenga kambi ya jeshi la majini na bandari.

Forum

XS
SM
MD
LG