Jumuiya ya madaktari inayojishirikisha na harakati za maandamano imesema waandamanaji 178 walijeruhiwa Jumamosi na wamevishutumu vikosi vya usalama kutumia risasi za moto.
Maafisa wa Sudan hata hivyo wamesema maafisa wa polisi 58 wameripoti majeruhi wakati wa maandamano.
Pia maafisa hao wameongeza kuwa zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika mji mkuu.
Maandamano ya kuunga mkono demokrasia yaliyofanyika Jumamosi yameshuhudia maelfu ya watu wakiwasili katika makazi ya rais kwa mara ya pili kwa wiki, wakipeperusha bendera na kuimba nyimbo kupinga jeshi.
Walikutana na vikosi vya usalama na gesi ya machozi ilitumika kwa ajili ya kuwatawanya.
Pia waliandamana katika miji kadhaa ikiwemo port sudan, ambako kulikuwa na taarifa kwamba watu walikamatwa na kupigwa.