Mamlaka ya Sudan iliimarisha usalama katika mji mkuu, Khartoum, na mji pacha wa Omdurman, na kuweka vizuizi katika majengo ya serikali na kijeshi.
Maandamano ya Jumapili yanaadhimisha mwaka wa tatu tangu kuanza kwa uasi ambao hatimaye ulilazimisha kuondolewa na jeshi kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir na serikali yake ya Kiislamu mwezi Aprili mwaka 2019.
Sudan kisha ikafuata njia dhaifu ya demokrasia na kuongozwa na serikali ya pamoja ya kijeshi na kiraia. Mapinduzi ya Oktoba 25 yamepelekea shida katika kipindi cha mpito na kusababisha maandamano yasiyokwisha mitaani.