Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 16:14

Polisi wa Sudan wafyatua mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji


Waandamanaji Sudan wakipinga utawala wa kijeshi
Waandamanaji Sudan wakipinga utawala wa kijeshi

Waandamanaji hao waliandamana kutoka wilaya mbalimbali za mji mkuu, wengi wakiwa wamebeba bendera za taifa na wakiimba “Hapana kwa utawala wa kijeshi” na "jeshi linaweza kukusaliti, lakini mitaa haitakusaliti kamwe"

Polisi wa Sudan walifyatua mabomu ya gesi ya kutoa machozi leo Jumatatu wakati maelfu ya watu walipoandamana karibu na makazi ya rais mjini Khartoum dhidi ya serikali inayo-ongozwa na jeshi, walioshuhudia waliliambia shirika la habari la AFP.

Waandamanaji hao waliandamana kutoka wilaya mbalimbali za mji mkuu, wengi wakiwa wamebeba bendera za taifa na wakiimba “Hapana kwa utawala wa kijeshi” na "jeshi linaweza kukusaliti, lakini mitaa haitakusaliti kamwe". Jenerali wa cheo cha juu huko Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, alinyakua mamlaka na kumuweka kizuizini Waziri Mkuu Abdalla Hamdok hapo Oktoba 25 baada ya tukio hilo kulaaniwa kimataifa na kuwepo maandamano makubwa, jenerali huyo alimrejesha madarakani Hamdok katika makubaliano yaliyotiwa saini Novemba 21.

Waandamanaji Sudan wakipinga utawala wa kijeshi
Waandamanaji Sudan wakipinga utawala wa kijeshi

Wakosoaji waliyashutumu makubaliano hayo na kumshutumu Hamdok kwa usaliti huku wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wakiapa kudumisha shinikizo kwa mamlaka ya kijeshi na kiraia. Jenerali huyo mkuu amesisitiza kwa muda mrefu, hatua ya jeshi kwamba sio mapinduzi, bali ni hatua ya kurekebisha mpito kuelekea demokrasia kamili ambayo ilianza na kuondolewa kwa rais wa kiimla, Omar al-Bashir hapo mwaka 2019.

XS
SM
MD
LG