Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:24

Ushirikiano wa kijeshi na Ufaransa mashakani Burkina Faso


FILE - Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Paris, Julai 9, 2021.(Photo by STEPHANE DE SAKUTIN / POOL / AFP)
FILE - Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Paris, Julai 9, 2021.(Photo by STEPHANE DE SAKUTIN / POOL / AFP)

Muungano wa mashirika ya kutetea raia nchini Burkina Faso yenye wanachama 72 yamefanya mkutano wa hadhara kutaka kusitishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hiyo na Ufaransa.

Muungano huo umetaka viongozi wa Burkina Faso kumaliza ushirikiano na jeshi la Ufaransa na badala yake kushirikiana na Russia katika kumaliza ugaidi.

Ousmane Ouedraogo, naibu wa katibu mkuu wa muungano huo, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kwa miaka mingi Ufaransa imekuwa Burkina Faso kwa madai kwamba inapigania maslahi ya watu wa Burkina Faso lakini yanayoonekana ni kinyume.

Naibu katibu mkuu Ouedraogo ameeleza haya: "Tunastahili kupanua mikakati yetu, tumechagua nchi kadhaa ambazo zimetajwa lakini tunaifkiria Russia kwa sababu kote duniani, Russia ndio nchi pekee ambayo imefanikiwa kupambana na magaidi nchini Syria, Venezuela, jamhuri ya Afrika ya kati na katika nchi jirani ya Mali ambapo tunaona matumaini makubwa.

Katika miezi ya hivi karibuni, Russia imekuwa ikiimarisha ushirikiano wake na mataifa kadhaa ya Afrika kupitia kundi binafsi la Wagner, kwa lengi la kupambana na makundi ya kigaidi na wapiganaji wenye misimamo mikali katika nchi kama Jamhuri ya Afrika ya kati na Mali.

Muungano wa mashirika ya kiraia ulindwa baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Januari 24, yaliyomuondoa madarakani rais Roch Marc Christian Kaboré.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG