Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 09:16

Upinzani nchini Comoros watupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa bunge


Rais wa Comoros Azali Assoumani akipiga kura kwenye kituo cha kura huko Mitsoudje, Januari 12, 2025, katika uchaguzi wa bunge. Picha ya AFP
Rais wa Comoros Azali Assoumani akipiga kura kwenye kituo cha kura huko Mitsoudje, Januari 12, 2025, katika uchaguzi wa bunge. Picha ya AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Comoros Jumatatu alitupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa wabunge, ambao ulisusiwa kwa kiasi kikubwa na wapinzani, kwa madai ya “udanganyifu mkubwa”.

Vyama vingi vya upinzani vilikataa kushiriki katika uchaguzi wa Jumapili kwa madai kuwa uchaguzi huo wa duru mbili kuwachagua wabunge 33 haukuwa na uwazi.

“Uchaguzi uligubikwa na udanganyifu mkubwa, kujaza masunduku ya kura na katika vituo kadhaa, kulikuwa na kura nyingi zaidi kuliko watu waliojiandikisha,” alisema Daoud Abdallah Mohamed, waziri wa zamani wa mambo ya ndani na kiongozi wa muungano wa upinzani.

Tume huru ya uchaguzi katika kisiwa cha Anjouan chenye idadi kubwa ya watu, iliwatangaza kama washindi wagombea 12 wa chama tawala cha the Renewal of the Comoros ( CRC).

Tume hiyo imesema wagombea wa CRC walipata kati ya asilimia 60 na 100 ya kura, huku idadi ya waliopiga kura ikiwa asilimia 70.

Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika tarehe 16 Februari.

Mohamed amesema muungano wao United Opposition “hautoshiriki”.

Forum

XS
SM
MD
LG