Juhudi za upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo za kupata mgombea mmoja wa kiti cha urais,zimevunjika kufuatia msimamo wa Etienne Tshisekedi wa kujitangaza kuwa mgombea wa chama chake cha UDPS.
Mpinzani mwingine Vital Kamerhe ambaye amesikitishwa na hatua hiyo ya Tshisekedi amesema lengo la upinzani hivi sasa ni kumwangusha rais aliyeko madarakani hivi sasa Bw. Joseph kabila kupitia uchaguzi licha ya tofauti miongoni mwa wapinzani.
Jumatano vyama vidogo kama vinane hivi, vimemuunga mkono Etienne Tshisekedi kama mgombea wa kiti cha urais na kuunda vuguvugu jipya la kumuunga mkono.