Kiongozi wa chama cha Union pour la Nation Congolaise, UNC, Bw Vital Kamerhe, amesema, ni jambo zuri kwa serikali kukamilisha uchunguzi wake kutokana na shambulio la Jumapili tarehe 27 February dhidi ya Ikulu ya Gombe mjini Kinshasa, lakini anaongezea kusema kwamba ni lazima ukweli wote ufahamike.
Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Kinshasa, Spika huyo wa zamani wa bunge la Kongo amesema. ni jambo la kushangaza kuona kwamba "wavamizi walivuka kituo cha kwanza cha ukaguzi, na kufika hadi kituo cha pili kwa kutumia mapanga na visu".
Bw Kamerhe anasema upinzani utakutana na kutoa msimamo wao wa pamoja baada ya kufahamu vyema walohusika na kwanini hakuna usalama wa kutosha kumlinda rais.