Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 18:42

UN yaituhumu Australia kwa kukiuka majukumu ya kulinda haki za binadamu


FILE - Baraza la Haki za Binadamu la U.N. likikutana Geneva, March 2, 2022. On Oct. 6, 2022, Baraza hilo lilipiga kura kuzuia mswaada wa kufanya mjadala juu ya madai ya ukandamizaji wa haki za binadamu unaofanywa na China dhidi ya watu wa kabila la Uyghurs huko Xinjiang.
FILE - Baraza la Haki za Binadamu la U.N. likikutana Geneva, March 2, 2022. On Oct. 6, 2022, Baraza hilo lilipiga kura kuzuia mswaada wa kufanya mjadala juu ya madai ya ukandamizaji wa haki za binadamu unaofanywa na China dhidi ya watu wa kabila la Uyghurs huko Xinjiang.

Umoja wa Mataifa unaituhumu Australia kwa kukiuka jukumu lake la kulinda haki za binadamu baada ya kusitisha ziara katika magereza. Wakaguzi wa UN wanasema mamlaka katika majimbo ya Australia ya New South Wales na Queensland wamewanyima ruhusa ya kuingia katika magereza mbalimbali.

Australia iliidhinsiha Makubaliano ya Hiari ya Umoja wa Mataifa ya Mkataba Dhidi ya Mateso mwaka 2017.

Wakaguzi kutoka kamati ndogo ya UN inayosimamia kuzuia mateso iliwasili Australia wiki iliyopita kufanya ziara za kushtukiza katika jimbo, maeneo na magereza ya serikali kuu kwa siku zaidi ya 12.

Katika taarifa ya Mwezi Juni 2022, UN ilisema kamati hiyo itatembelea Australia, Bosnia na Herzegovina, Ecuador na Uturuki katika nusu ya pili ya mwaka 2022

Jukumu la Kamati hiyo ni “ kuwalinda watu wanaonyimwa uhuru wao katika… siyo tu magerezani lakini vituo vya polisi, taasisi za ugonjwa wa akili, kambi za wakimbizi zilizofungwa na vituo vinavyowashikilia wahamiaji.”

Hata hivyo, mamlaka katika majimbo ya Australia ya New South Wales na Queensland waziri wa jela wa New South Wales Geoff Lee aliwaambia waandishi Jumatatu kuwa watu hawawezi kuruhusiwa “kuranda randa kama wanavyopenda” jela za jimbo na kuwa UN “iendee huko Iran kutazama ukiukaji wa haki za binadamu.”

UN hivi sasa imesema kuwa Australia imekiuka majukumu yake chini ya masharti ya mateso.

Dr. Alice Edwards, who is a U.N. Special Rapporteur on Torture and other Cruel, Inhuman or Degrading Treatment or Punishment, told the Australian Broadcasting Corp. on Monday that Australian authorities were going against an international system of scrutiny.

Dr. Alice Edwards, ambaye ni mwakilishi maalum wa UN katika masuala ya mateso na ukatili mwingine, unyama au adhabu au matendo ya udhalilishaji, ameliambia shirika la utangazaji la Australia Jumatatu kuwa mamlaka nchini Australia walikuwa wanakwenda kinyume na mfumo wa uchunguzi wa kimataifa.

“Hili ni tukio la kusikitisha kwa hali yoyote ile. Nafikiri pengine kile ambacho New South Wales imshindwa kutambua ni kuwa hii ni sehemu ya mfumo wa kimataifa,” alisema Edwards. “Ni kitu kikubwa zaidi kuliko wao na pia nayatahadharisha majimbo kudharau vitu vidogo vinavyoweza kupelekea kutokea tatizo kubwa zaidi.”

Serikali kuu ya Australia imeisihi serikali za majimbo yote kuheshimu ukaguzi wa UN.

XS
SM
MD
LG