Hayo ameyasema Mkuu wa masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura Martin Griffiths katika taarifa yake mwishoni mwa wiki.
"Vita vizito vimeuharibu mji mkuu Khartoum na Darfur tangu kuanza katikati ya Aprili na sasa vimeenea huko Kordofan.
Vita nchini Sudan vinachochea hali ya dharura ya kibinadamu iliyovuka viwango vya kawaida," amesema Griffiths.
Kulingana na taarifa hiyo ya UN katika mji mkuu wa Kordofan Kusini, Kadugli, akiba ya chakula imemalizika, huku mapigano na vizuizi vya barabarani vikiwazuia wafanyakazi wa misaada kuwafikia watu wenye njaa.
Katika mji mkuu wa Kordofan Magharibi, El Fula, ofisi za misaada ya kibinadamu zimevamiwa na bidhaa zote kuibiwa, taarifa imeeleza.
Griffiths amesema kuwa: “Nina wasiwasi mkubwa pia kuhusu usalama wa raia katika Jimbo la Al Jazira, huku vita vikisogea karibu na eneo linalozalisha chakula cha nchi nzima nchini Sudan.”
Kadiri vita vinavyoendelea, ndivyo vinavyozidi kuleta athari mbaya zaidi.”
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa baadhi ya sehemu zimeishiwa chakula na maelfu ya watoto wana utapiamlo na wako hatarini kupoteza maisha iwapo hawatapata matibabu.
Kulingana na taarifa ya UN maradhi ya kuambukiza yanaenea, na kuhatarisha maisha ya watu, hususan wale ambao tayari wamedhoofika kutokana na utapiamlo.
Pia imeeleza kuwa maradhi ya surua, malaria, kifaduro, homa ya dengue na kuharisha yameripotiwa kote nchini. Watu wengi hawawezi kufikia huduma za afya.
Forum