Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:26

Mzozo wa kibinadamu nchini Sudan unaiangamiza nchi hiyo; anasema Griffiths


Martin Griffiths, mkuu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa mataifa. Jan. 25, 2023.
Martin Griffiths, mkuu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa mataifa. Jan. 25, 2023.

Mkuu wa kitengo cha misaada katika Umoja wa Mataifa amesema kutokana na mapigano na vizuizi vya barabarani, akiba  ya chakula imekwisha  kabisa katika mji mkuu wa Kordofan Kusini, Kadugli na wafanyakazi wa misaada wamezuiwa kuwafikia watu wenye njaa

Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema Ijumaa kuwa mzozo nchini Sudan na mzozo wa kibinadamu ambao umeibuka nchini humo unatishia kuiangamiza nchi nzima.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya kibinadamu Martin Griffiths, amesema mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces ambavyo vimeuharibu mji mkuu Juba, Khartoum na Darfur tangu kati-kati ya mwezi Aprili yameenea kusini mashariki mpaka jimbo la Kordofan.

Mkuu wa kitengo cha misaada katika Umoja wa Mataifa amesema kutokana na mapigano na vizuizi vya barabarani, akiba ya chakula imekwisha kabisa katika mji mkuu wa Kordofan Kusini, Kadugli na wafanyakazi wa misaada wamezuiwa kuwafikia watu wenye njaa.

Katika mji mkuu wa Kordofan Magharibi, El Fula, ofisi za misaada ya kibinadamu zimeporwa na vifaa vimeibiwa. Mkuu huyo wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa raia katika jimbo la Al Jazira, wakati mzozo huo ukielekea kuikumba Sudan ambayo ilikuwa mhimili wa chakula katika eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG