Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:07

Umri wa kuishi nchini Marekani waongezeka mwaka 2022


FILE - Watoto waliozaliwa wakiwa katika kituo cha kuwafuatilia afya za watoto waliozaliwa katika wiki sita za kwanza huko eneo la juu la New York, Feb. 16, 2017.
FILE - Watoto waliozaliwa wakiwa katika kituo cha kuwafuatilia afya za watoto waliozaliwa katika wiki sita za kwanza huko eneo la juu la New York, Feb. 16, 2017.

Umri wa kuishi nchini Marekani umeongezeka mwaka jana – kwa zaidi ya mwaka – lakini siyo karibu na ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19.

Kuongezeka kwa umri wa kuishi mwaka 2022 hasa kulitokana na kuondoka kwa janga la COVID, watafiti wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maambukizi ya Maradhi walisema Jumatano.

Lakini pamoja na ongezeko kubwa, umri wa kuishi Marekani umerejea tu katika kiwango cha miaka 77, miezi sita – hali iliyokuwepo miongo miwili iliyopita.

Umri wa kuishi ni makadirio ya wastani wa idadi ya miaka ya mtoto kuzaliwa katika mwaka fulani akitarajiwa kuishi, ikichukuliwa kuwa matukio ya vifo kwa muda huo yatabakia kama yalivyo

Muhtasari wa Takwimu zilizochukuliwa zinakadiriwa kuwa moja ya vipimo muhimu vya afya ya wananchi wa Marekani.

Mahesabu ya 2022 yaliyotolewa Jumatano ni ya awali, na yanaweza kubadilika kidogo wakati mahesabu hayo yakikamilishwa.

Kwa miongo kadhaa, umri wa kuishi uliongezeka kidogo karibuni kila mwaka. Lakini muongo mmoja uliopita, mwelekeo huo ulibakia ulivyo na hata kushuka katika baadhi ya miaka – hali iliyoelezewa kwa kiwango kikubwa kusababishwa na vifo vya matumizi mabaya ya dawa na kujiua.

Baadaye vikaja virusi vya corona, ambavyo vimewauwa zaidi ya watu milioni 1.1 nchini Marekani kuanzia mapema 2020. Kipimo hicho cha maisha marefu ya Wamarekani kiliporomoka, kikishuka kutoka miaka 78, miezi 10 mnamo mwaka 2019 kufikia miaka 77 mwaka 2020, na baadaye kufikia miaka 76, miezi 5 mwaka 2021.

“Kimsingi tumepoteza miaka 20 tuliyopiga hatua mbele,” alisema Elizabeth Arias wa CDC.

Kushuka kwa vifo vya COVID-19 kulipelekea mabadiliko ya kuongezeka kwa umri wa kuishi mwaka 2022.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG