Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:51

Ukraine inaishtumu Russia kushambulia meli ya nafaka


Meli ya nafaka ya Ukraine kwenye pwani ya Black Sea, mashariki mwa mji wa Odessa.
Meli ya nafaka ya Ukraine kwenye pwani ya Black Sea, mashariki mwa mji wa Odessa.

Ukraine Alhamisi iliishtumu Russia kwa kutumia makombora ya kimkakati kushambulia meli ya nafaka ya kiraia katika shambulizi la kombora katika bahari ya Black Sea karibu na Romania, nchi mwanachama wa NATO, na kuzidisha mvutano kati ya Moscow na muungano huo wa ushirika wa kijeshi.

Rais Volodymyr Zelenskiy alisema meli hiyo iliyokuwa inasafirisha nafaka kuelekea Misri ilishambuliwa usiku wa Jumatano na kombora la Russia mara tu baada ya kuondoka kwenye eneo la bahari ya Ukraine.

Alisema hakuna vifo vilivyotokea.

Balozi wa Marekani nchini Ukraine “alilaani vikali” shambulizi hilo na kusema Russia ilihusika. Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema tukio hilo ni “ukumbusho mkubwa” wa vitisho ambavyo meli za kiraia bado zinakabiliana navyo katika bahari ya Black Sea.

Russia haikutoa mara moja maelezo kuhusu tukio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG